Yule beki mrefu wa Ruvu
Shooting, George Michael ambaye alijizolea umaarufu kwa kuwasimamisha mastraika
wa Simba na Yanga katika raundi ya kwanza Ligi Kuu Bara, amevunjika mguu na
imeelezwa huenda akakosa mzunguko wote wa pili.
Msemaji wa Ruvu, Masau
Bwire amesema Michael alivunjika mguu wakati wa mazoezi ya timu hiyo juzi
Jumatano kwenye Uwanja wa Mlandizi, hali aliyosema ni pigo kubwa, hususan timu
yao itapokutana na vigogo raundi ya pili.
Beki huyo ndiye pia
aliyempa wakati mgumu Amissi Tambwe wa Simba wakati timu hizo zilipokutana.
“Alikuwa katika harakati
za kukaba, huenda akawa nje kwa muda mrefu zaidi. Bado hatutajua ni lini
atarejea maana hajapata vipimo na alitarajiwa kupimwa Alhamisi (jana), lakini
uhakika nilionao ni kwamba tutamkosa raundi ya pili yote,” alisema Bwire.
Wakati huohuo alisema leo
kikosi chao kitakuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Friends Rangers kwa ajili
ya kujiandaa na raundi ya pili itakayoanza kutimua vumbi Januari 25.
0 COMMENTS:
Post a Comment