Kukosekana kwa kiungo
mzoefu Athumani Idd ‘Chuji’ kwenye msafara wa Yanga uliotua nchini Uturuki kwa
ajili ya kambi, kumewasikitisha wachezaji wenzake kadhaa ambao wamesema
wanatamani wangekuwa naye.
Beki na nahodha wa Yanga,
Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema Chuji ni mchezaji muhimu hasa katika mechi za
kimataifa, ndiyo maana kukosekana kwake katika safari kumekuwa ni pigo.
“Naamini pengo la Chuji
litazibwa lakini si kwa urahisi hivyo kwa sababu angekuwa msaada mkubwa kwenye
mechi za kimataifa, ni mzoefu na mkongwe pia kwenye soka, hivyo vinachangia
umuhimu wake kwa kiasi kikubwa,” alisema Cannavaro.
Naye mshambuliaji wa
Yanga, Hamis Kiiza, amesema anaamini umuhimu wa Chuji ni mkubwa lakini hawezi
kuingilia amri ya uongozi.
“Sina la kusema kwa kuwa
uongozi wa timu ndiyo umefanya hilo lakini umuhimu wake uwanjani unajulikana,”
alisema Kiiza.
0 COMMENTS:
Post a Comment