Chelsea imeipiga bao Liverpool na kumsainisha mshambuliaji hatari
wa FC Basle, Mohamed Salah.
Chelsea imemwaga pauni milioni 11 kumnasa raia huyo wa Misri
ambaye amekuwa akiisumbua kila wanapokutana kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Salah sasa atafunga safari kutoka Uswiss na kuhamia London,
England ambako ndiyo makao makuu ya Chelsea.
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers alionyesha nia ya kumnasa
mshambuliaji huyo, lakini kuchelewa kwake, amekuta mwana si wake.
0 COMMENTS:
Post a Comment