Wakala wa Wayne Rooney leo amefanya mazungumzo na uongozi wa Manchester
United kuhusiana na kubaki kwa mchezaji huyo.
MAzungumzo kati ya Paul Stretford ambaye ni wakala wa Rooney au
Wazza na bosi, Ed Woodward yalikuwa ni kujadili kuongeza mkataba ambao umebaki
miezi 18.
Imeelezwa Man United imeshituka na kuona ijadili mkataba mapema
kwa kuwa Rooney anaonekana kuanza kuvutiwa na Chelsea pamoja na Real Madrid
ambazo zimeonyesha nia ya kumnasa.
Bado haijajulikana hasa mwafaka waliofikia na nini kinachotakiwa
lakini inaonekana Man United imepania kumbakiza Wazza kwa muda mrefu zaidi
0 COMMENTS:
Post a Comment