Nahodha na beki wa pembeni wa Simba, Said Nassor ‘Chollo’, leo Ijumaa anatarajia
kupelekwa kwenye Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) kwa ajili ya uchunguzi zaidi
wa kiafya, hivyo kuenguliwa kwenye kikosi kitakachoivaa Rhino Rangers ya
Tabora, keshokutwa Jumapili.
Chollo
aliyerejea hivi karibuni baada ya kukaa nje kwa muda kutokana na maumivu ya
nyama za paja za mguu wa kulia, amepata maumivu mapya ya nyonga juzi alipokuwa
mazoezini.
Daktari
wa Simba, Yassin Gembe amesema kuwa kutokana na maumivu
makali aliyokuwa nayo beki huyo pamoja na kuumia kwake mfululizo katika siku za
hivi karibuni, wameamua kumfanyia vipimo vya kina vya mwili mzima kujua undani
wa majeraha yake hayo ya mara kwa mara.
“Chollo
ataikosa mechi ya Rhino kutokana na maumivu ya nyonga aliyokuwa nayo na Ijumaa
(leo) tutampeleka MOI kwa ajili ya vipimo vya kina kujua nini chanzo cha kuwa
majeruhi mara kwa mara,” alisema Gembe.
0 COMMENTS:
Post a Comment