January 12, 2014


Pamoja na kuachwa safari ya Uturuki, kiungo Athumani Iddi ‘Chuji’ amekuwa akiendelea na mazoezi makali jijini Dar.

Chuji amekuwa akifanya mazoezi kama wachezaji walioko katika kambi kwa ajili ya kujiandaa na Ligi Kuu.

Rafiki wa karibu wa Chuji amesema kiungo huyo amekuwa akifanya mazoezi mara mbili kwa siku kujifua kabla ya Ligi Kuu Bara mwishoni mwa mwezi huu.

“Unajua amepeleka barua ya kuomba msamaha, kama atasamehewa basi atarudi kwenye kikosi na ni vizuri awe fiti.

“Jamaa amekuwa akifanya mazoezi makali ile mbaya, unaweza kudhani yuko kambini na wachezaji wengine,” alisema rafiki yake huyo wa karibu.


Alipoulizwa juzi, jana mchana alisema: “Ngoja nimalize mazoezi ya jioni halafu tutaongea wangu.” Halafu simu yake haijapatikana hadi leo.

Chuji alisimamishwa kwa muda usiojulikana kwa madai ya utovu wa nidhamu, kocha kubwa liliolezwa ni kwenda nyumbani mara tu baada ya kutolewa wakati wa mapumziko wakati Yanga ikiivaa Simba katika mechi ya Nani Mtani Jembe, Desemba 21, mwaka jana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic