OMOG SIKU ALIPOKABIDHIWA MIKOBA YA KUINOA AZAM FC, KULIA NI MWENYEKITI WA KLABU HIYO, MZEE SAID |
Kocha Joseph Omog wa Azam FC amesema
kikosi chake bado kina nafasi ya kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu Bara.
Omog raia wa Cameroon amesema
kutolewa kwenye michuano ya Mapinduzi kunaweza kuwa faida kubwa kwao kwenye
Ligi Kuu.
“Kama umekosea na ukakubali na
kujifunza, basi unakuwa bora sana, sisi tunalitegemea hilo.
“Tukitumia njia hiyo vizuri, basi
kuna nafasi ya kufanya vizuri zaidi kwenye ligi,” alisema Omog.
Azam FC ilivuliwa ubingwa wa
Mapinduzi baada ya kuchapwa kwa mabao 3-2 na KCC ya Uganda.
Sasa Waganda hao watacheza fainali
kesho mjini Zanzibar dhidi ya Simba ambao pia waliwang’oa Waganda wengine URA.
0 COMMENTS:
Post a Comment