Uongozi wa Coastal Union umekataa tiketi za elektroniki kutumika kwenye Uwanja wa
Mkwakwani kwa kuwa hakuna kati yao anayejua matumizi ya teknolojia hiyo.
Uwanja wa
Mkwakwani uliopo Tanga ambao unatumiwa na Mgambo na Coastal, ni miongoni mwa
viwanja ambavyo vimefungwa mashine za kielektroniki.
Katibu
Mkuu wa Coastal, Kasim El Siagi amesema uwanja huo haujawa tayari kwa matumizi
ya teknolojia hiyo licha ya ujenzi wa mashine hizo kuwekwa kwenye milango
miwili kati ya mitano iliyopo uwanjani hapo.
“Hakuna
semina yoyote iliyotolewa juu ya matumizi ya mashine hizo, tujiulize mamia
wanaotumia lango kuu wanafanyaje na milango yao haijawekwa mashine? Mpaka sasa
meneja wa uwanja hajui na hata hao CRDB wapo kimya.
“Tunaomba
mpango huu uachwe mpaka tucheze mechi mbili (dhidi ya Oljoro na Yanga) kisha
vikao vya wadau hapa Tanga vifanyike watu waelimishwe,” alisema El Siagi.
0 COMMENTS:
Post a Comment