Rais wa Barcelona, Sandro
Rosells ametangaza
kuachia ngazi katika klabu hiyo.
Rosells ametangaza kuachia
ngazi kuachia ngazi kwenye kikao cha dharura cha bodi kilichofanyika leo jijini
Barcelona.
Imeelezwa sababu za kuachia ngazi kwa Rosells kumetokana na sakata la uhamisho wa mshambuliaji
Neymar kutoka Brazil.
Hivi karibuni, kumekuwa na taarifa zilitumika
fedha nyingi zaidi ya ilivyotangazwa ili kumnasa Neymar kutoka Brazil.
Lakini mambo yakaenda kwa uficho hadi
ilipojulikana na kusababisha kauli za kujikanganya kuanza kujitokeza.
Josep Maria Bartomeu sasa
atachukua nafasi ya Rosells ambaye amechukua
uamuzi ambao haukuwa umetegemewa hapo kabla.
0 COMMENTS:
Post a Comment