Taarifa za Emmanuel Okwi kuzuiwa kuichezea Yanga zilikuwa furaha kubwa kwa mashabiki wa
Simba waliojitokeza katika mazoezi ya timu yao juzi kwenye Uwanja wa Kinesi
jijini Dar.
Okwi
ambaye yupo Yanga, amezuiwa kuichezea timu hiyo na Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) kutokana na kuwa na kesi tatu tofauti juu ya uhamisho wake kutoka Simba
kwenda Etoile ya Tunisia, kisha kusajiliwa SC Villa ya Uganda na baadaye kutua
Yanga.
SALEHJEMBE iliwashuhudia mashabiki hao wakiimba
kwa sauti kubwa ‘Okwi! Okwi! Okwi!’ Huku mazoezi ya Simba yakiendelea, hali
iliyozua taharuki kwa wengine ambao hawakuwa na taarifa.
“Muacheni
akutane na rungu la Fifa si anajifanya anajua sana! Tatizo wachezaji wetu wa
Kiafrika wanapenda sana hela za papo kwa papo, sasa zitamtokea puani,”
alisikika shabiki mmoja huku akiungwa mkono na wengine wengi waliokuwa wakitoa
maneno ya kejeli kwa Yanga na Okwi aliyekuwa mchezaji wa Simba.
Kamati ya Hadhi ya Wachezaji ya TFF, imesimamisha usajili wa Okwi hadi hapo itakapopata ufafanuzi kutoka Fifa.
Tayari suala lake limeanza kushughulikiwa na maana yake atakosa mechi ya Jumamosi dhidi ya Ashanti.
Okwi anawasili nchini kesho alfajiri akiwa na kikosi cha Yanga kilichokuwa kimeweka kambi nchini Uturuki.
0 COMMENTS:
Post a Comment