Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic
amesema mechi dhidi ya KCC ya Uganda haitakuwa lahisi na lazima wawe makini.
Simba itaivaa KCC katika mechi ya
fainali ya Kombe la Mapinduzi, keshokutwa Jumatatu kwenye Uwanja wa Amaan mjini
Zanzibar.
Logarusic amesema wachezaji wa Simba
wanapaswa kuwa makini na KCC kwa kuwa ina kikosi bora.
“Wote tunajua ni wazuri, utaona
tulipokutana nao tulitoka sare ya bila kufungana.
“Tunakutana mara ya pili, lazima itakuwa
mechi ngumu na kila upande tayari unajua nini cha kufanya,” alisema.
Mechi hiyo inasubiriwa kwa hamu sana na
wadau wengi nchini na wengi watasafiri kwenda mjini Zanzibar kuishuhudia mechi
hiyo.
Simba imeingia fainali baada ya kuichapa
URA ya Uganda kwa mabao 2-0 wakati KCC ikawavua ubingwa Azam FC kwa kuwatundika
mabao 3-2.
0 COMMENTS:
Post a Comment