January 12, 2014

VAN PLUIJM WAKATI AKIWA BEREKUM CHELSEA

Johannes Franciscus ‘Hans’ van der Pluijm amesema haijui Yanga vizuri lakini atavuta subira.


Kocha huyo raia wa Uholanzi amesema iwapo atakuja jijii Dar es Salaam ndiyo atatoa majibu.
Yanga imemtaka kocha huyo wa zamani wa Berekum Chelsea atue jijini Dar leo kwa ajili ya mazungumzo.
Lakini hofu ilikuwa ni safari za ndege na huenda akatua kesho kama mambo hayatakwenda vizuri.

Wakala wake aitwaye Thomas amesema mtu mzima huyo anaweza kutua Dar es Salaam leo au kesho.
“Lakini hajui lolote kuhusiana na Yanga, hivyo vuta subira, kila kitakachotokea tutawaeleza,” alisema.
Huenda Thomas akaongozana na van der Pluijm kuja nchini kama pia atapa tiketi.

Kocha huyo aliwahi kuiongoza Berekum Chelsea ya Ghana kuwapa ‘shughuli’ Al Ahly na Zamalek za Misri, pia TP Mazembe ya DR Congo. 

Gazeti maarufu la michezo laCHAMPIONI lilikuwa la kwanza kuandika kuhusiana na kocha huyo.

CHAMPIONI la juzi Ijumaa liliandika kuwa kocha huyo Mholanzi ndiye amekuwa chaguo namba moja wa Yanga na si wale makocha wengine ambao walikuwa wametangazwa hapo awali au kuandikwa na magazeti mengine.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic