Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm
amesema baada ya mechi tatu, kikosi chake kitaimarika zaidi.
Van Der Pluijm, raia wa Uholanzi amesema
amebahatika kukaa na kikosi hicho kwa wiki moja tu akifanya nao kazi na ameona
kuna wachezaji wengi wenye vipaji lakini anahitaji muda kidogo.
“Kweli nahitaji muda kidogo, lakini hauwezi
kuwa muda mrefu sana. Tutakuwa katika hali nzuri zaidi ya sasa pia kuna
mabadiliko kadhaa nitakuwa nimefanya,” alisema.
Kocha huyo aliyewahi kufundisha soka
nchini Ghana, amesema baada ya mechi tatu, atakuwa na uhakika wa nini atafanya
katika kikosi hicho kwa kuwa tokea ameanza si muda mrefu.
Mechi yake ya kwanza ya mashindano
ilikuwa ni pale Yanga ilipovaa Ashanti United katika mechi ya kwanza ya
mzunguko wa pili na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 ingawa haikunyesha soka la
kuvutia.
0 COMMENTS:
Post a Comment