January 30, 2014


LOGA AKIPANGA MIKAKATI NA KIEMBA

Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic 'Loga' amesema anataka kuwa na wachezaji wenye moyo wa ushindani na wasiokubali kushindwa.

Loga amesema anaamini kuwa na washindani katika kikosi chake ni jambo la msingi zaidi, na haamini watu wanaokata tamaa mapema.
“Kama unakata tamaa mapema, basi hauwezi kufanya kazi na mimi. Nataka wapambanaji.

“Katika maisha kuna mawimbi, hauwezi kusafiri baharini bila ya kukutana na mawimbi. Ukikata tamaa mapema, hautafika unapokwenda.”
Loga anaamini kuwa mmoja wa makocha wakorofi lakini amekuwa akisifika kwa kusimamia suala la nidhamu.

Tokea ametua Simba, inaonekana suala la nidhamu limeimarika zaidi na watukutu wamekuwa na hofu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic