Kocha Mkuu wa Tanzania
Prisons, David Mwamwaja, ameongeza kasi ya mazoezi ambapo sasa watafanya mara
tatu kwa siku, ikiwa ni mkakati wa kujiweka fiti kabla ya kuanza kwa mzunguko
wa pili wa Ligi Kuu Bara.
Kocha huyo amesema mazoezi
yatakuwa yakifanyika mara tatu kwa siku ambapo ni asubuhi, mchana na jioni.
"Nafurahi kuona
Peter Michael ameanza kufanya mazoezi na anaendelea vizuri kwani alikuwa
anaumwa ila kwa sasa hali yake imetengemaa na anafanya vizuri, nina imani ataendelea
kufanya vizuri kama msimu uliopita.
"Timu yangu inacheza
kwa kutegemeana, hatutegemei mtu mmoja, wachezaji wanaonyesha kuelewa mazoezi
yangu, hiyo inanipa moyo wa kufanya vizuri ligi itakapoanza,” alisema Mwamwaja.
Prisons inashika nafasi
ya pili kutoka chini katika msimamo wa ligi kuu, ambapo imeshinda mechi moja,
sare sita na kufungwa sita.
0 COMMENTS:
Post a Comment