Shrikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mwanzilishi
wa wa timu ya Oljoro JKT, Kanali Mmari kilichotokea jana (Januari 13 mwaka huu)
jijini Dar es Salaam.
Kanali
Mmari ambaye aliasisi timu hiyo na kuifikisha hadi kwenye Ligi Kuu ya Vodacom
amefia Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambapo alikuwa amelazwa baada ya
kupata ajali ya gari Chalinze mkoani Pwani, Januari Mosi mwaka huu.
Msiba
huu ni mkubwa kwa jamii ya mpira wa miguu kwani mbali kuasisi timu ya Oljoro
JKT alikuwa mhamasishaji mkubwa wa mchezo huo mkoani Arusha, hivyo mchango wake
tutaukumbuka daima.
TFF
tunatoa pole kwa familia ya marehemu Kanali Mmari, klabu ya Oljoro JKT, Jeshi
la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Arusha
(ARFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha
msiba huo mzito.
Bwana
alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina
0 COMMENTS:
Post a Comment