KOCHA mkuu wa klabu ya Yanga, Nasreddine Nabi amesema kuwa licha ya kustahili shangwe la kumfunga mtani wao Simba kwenye mchezo wao wa Jumamosi, lakini wanapaswa kuwa makini katika maandalizi yao kuelekea mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho, kwani anaamini Simba watakuja katika mchezo huo wakiwa na hasira zaidi.
Yanga juzi Jumamosi iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa katika dimba la Mkapa Dar es Salaam, ambapo ushindi huo umeifanya Yanga kufikisha pointi 70 baada ya kucheza michezo 32 na kuzidi kujiimarisha katika nafasi ya pili ya msimamo.
Baada ya kumalizika kwa mchezo wa juzi wa kiporo, Simba na Yanga zinatarajiwa kukutana tena katika mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho la Julai 25, mwaka huu.
Akizungumzia mchezo huo wa fainali, kocha Nabi amesema: “Tunashukuru kwa ushindi ambao tumeupata dhidi ya Simba, nikiri wazi kuwa tulicheza dhidi ya timu nzuri na inayoundwa na wachezaji wengi bora, ushindi huu unatupa nafasi ya kusheherekea lakini hatupaswi kujisahau kwani tunakwenda kukutana nao katika mchezo mwingine wa kombe la Shirikisho.
“Najua watakuja wakiwa na hasira
zaidi kuelekea mchezo huo, ili kutaka kulipa kisasi cha kupoteza mchezo wa
Jumamosi, hivyo tunapaswa kujipanga vizuri kuhakikisha tunafanya vizuri katika
michezo yetu miwili iliyosalia na kujipanga mapema kwa ajili ya mchezo wa
fainali Julai 25.”
Waamuzi kuwa makini ni moja ya vitu vya msingi Sana ili apatikane mshindi wa halali ambaye hata akienda kushindana kimataifa ataonesha kuwa ni bingwa wa kweli
ReplyDeletetungeomba hata waamuzi wa Burundi hawa wa kwetu ni kichefuchefu
DeleteKweli kabisa wamuzi wangekua fair huenda simba wangekua nafas ya tatu
ReplyDeleteKweli, walibebwa mechi nyingi tu
DeleteUna maana refa alikua anachukua mpira anautupia golin au acheni ushabiki zungumzia soka kama soka no mini cha kufanya ili makosa yasijirudie au tufanye nn ili tuweze kusonga mbele
DeleteMechi ya Yanga na Simba nani alibebwa na Refa?
DeleteAcha ushabiki mandazi hata mechi ya juzi wangekuwa fair yanga angefungwa
ReplyDeleteBora Simba nao wamejua udhaifu wa waamuzi, mechi nyingi walibebwa msimu yliopita hata msimu huu, angalieni mechi zilizopita
ReplyDeleteOngea kwa mifano halisi sio TU mechi zilizopita. Haya zimekuwaje sasa.?
ReplyDeleteMashabiki wengi wanacheza mpira kwa mdomo hvyo refa akifanya maamuzi yake wanaanza kulalama cha kuwashauri mashabik wenzangu tujaribu angalau kidogo kushiriki kucheza kwenye timu zetu za mtaani tuingie uwanjani at least dk 45 za kipind kimoja naamini kila mmoja ataelewa ni kwann refa anafanya hiv na nikanini hafanyi hiv
ReplyDelete