March 21, 2021

  


IMERIPOTIWA kuwa uongozi wa Klabu ya Al Merrikh ya Sudan umetinga Shirikisho la Soka Afrika, (Caf) kuripoti kuhusu suala ambalo wameliita ni kuhujumiwa na Klabu ya Simba ya Tanzania kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwenye mchezo wa marudio uliochezwa Machi 16, Uwanja wa Mkapa na Simba kushinda mabao 3-0, Klabu ya Al Merrikh iliweka wazi kuwa wachezaji wake 8 waliripotiwa kwamba wana Corona muda mfupi kabla ya mechi jambo ambalo walidai kwamba ni hujuma.

 Miongoni mwa wachezaji ambao wametajwa kuwa na Corona ni Abdul Rahman Karngou, Altaj Yaqoub, Bhakit Khamis, Ramadan Ajab, Tony, Bakir Al Madina, Saif Al-Damazin, Emad Abdul-Manim.

Al Merrikh wametinga ofisi za Caf na kupeleka majibu yao ambayo wanadai kwamba yalikuwa yaanaonyesha kwamba hakuna mchezaji mwenye Corona bali ilikuwa ni ujanja wa Simba kutaka kuihujumu timu hiyo.

11 COMMENTS:

  1. Wanetinga na majibu toka wapi, kwa nini majibu hayo hawakumpa kamisaa wa mechi husika? Nani aliwapima na wapi. Watulie vibonde tuu hao.

    ReplyDelete
  2. Walipocheza na simba kule sudan, wachezaji wao 5 walikutwa na corona, jee na huko simba aliwapima? Waanae kuchukua tahadhari inaelekea hawako serious na hii kitu halafu wanalaunu oponents

    ReplyDelete
  3. Huku CAF wawateua baadhi ya wachezaji wa Simba kwenye kikosi Cha mwezi huku wakimpongeza shabalala kwa kufanya vizuri kwenye mechi ya I Almerekh. Waliwafanyia unyama waghana wamesahau?

    ReplyDelete
  4. Kwani vipimo wanachikua klabu mwenyeji au ni maafisa wa CAF?!

    ReplyDelete
  5. Wa2ache namaixha ye2 simba bro inatakiwa ilalamike.kwann mechi ya simba sudan na al merrikh ilichezexha wachezaji wawili ambao walifungiwa nachama cha soka nchini humo kwa kosa la kusaini mikataba natimu mbili tofauti na wamechezeshwa?
    Je? Nan anahaki yakulalamika? Wa2ache bhana 2songe mbelee

    ReplyDelete
  6. Inaonesha waz kuwa al merrikh hawajielewi je wangelishinda hapa kwa mkapa wangelalamika na vip kuhus hiyo mikataba feki ya wachezaj wao wawili

    ReplyDelete
  7. Aliyepewa kapewa hata uende wapi ufanye nini huwezi kumpoka,chamsingi merikh mjipange kwa awamu ijayo na sio kuzusha mambo yasiyo na tija, mnapaswa kujiuliza swali moja tu mlivyopimwa kule sudani mpaka mkapatikana na Korona je pia mlihujumiwa? Fanyeni mambo kama wasomi mtashangaza ulimwengu wa soka.povu RUKSAAAAAA.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic