Mabingwa wa Afrika, Al Ahly wamewasili
jijini Dar es Salaam leo saa 12 alfajiri na kupokelewa na wenzao waliotanguliwa
pamoja na maofisa wa Ubalozi wa Misri nchini.
Kikosi kizima cha Al Ahly kimewasili
huku viongozi na wachezaji wakigoma kuzungumza na waandishi wa habari, badala
yake wakisisitiza wamechoka na safari.
“Sio sasa, hatuwezi kuzungumza, tuna
uchovu sana,” alisema mmoja wa viongozi.
Juhudi za waandishi kuwashawishi
wazungumze zilikwama na muda mwingi waliutumia kuwasisitiza wachezaji waende kwenye
basi lililoandikwa Kakore Trans kwa ajili ya kuondoka kwenda katika hoteli ya
Kempinsky jijini Dar ambako ndiyo watafikia.
0 COMMENTS:
Post a Comment