SWITA AKIMDHIBITI MESSI WA SIMBA |
Kiungo mchezeshaji wa JKT Ruvu
aliyefunga mabao mawili na kuiangamiza Simba Jumapili iliyopita, Emmanuel Swita,
amesema yupo tayari kurejea Yanga iwapo watamhitaji.
Kiungo huyo alicheza Yanga msimu wa
2007/2008 kabla ya kutolewa kwa mkopo kwenda Toto African hadi mkataba wake
ulipokwisha.
Swita
alisema wakati anaondoka Yanga hakuondoka kwa ubaya bali alitolewa kwa mkopo na
alishangaa kuona wapo kimya hivyo kuchukua hamsini zake, lakini sasa anatamani
kurudi.
“Nashukuru kwa kufunga mabao hayo, najua Simba
walidhani labda sisi kufungwa mabao sita na Prisons ni wepesi, kumbe tulikuwa
tumechoka tu.
“Lakini mimi kama kuna timu inanitaka,
hata kama ni Yanga nipo tayari kujiunga nayo, sina kinyongo,” alisema
Swita.
0 COMMENTS:
Post a Comment