Katika kuhakikisha inafanya maandalizi mazuri na yenye ubora kwa ajili ya kuikabili Al Ahly ya Misri kwenye mchezo wa Klabu Bingwa Afrika, timu ya Yanga imeamua kuweka kambi kwenye hoteli ambayo mara ya mwisho ilitumiwa na timu ya taifa ya Ivory Coast.
Yanga ipo Ledger Hotel, Kunduchi jijini
, Dar, iliyotumiwa na Ivory Coast iliyokuja na mastaa kibao kama Yaya Toure,
Salomon Kalou, Wilfried Bony na Gervinho.
Ivory Coast walikaa hapo wakati wakiwa
hapa nchini ajili ya mechi ya kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia ilipovaana
na Taifa Stars na kushinda 4-2.
Yanga imeanza kambi hiyo jana na itadumu
hapo mpaka Ijumaa, ambapo Jumamosi asubuhi wanatarajiwa kurejea katikati ya
jiji tayari kuwakabili Al Ahly, mabingwa watetezi wa mashindano hayo.
Pamoja na hayo Yanga itakuwa ikifanya
mazoezi yake kwenye Uwanja wa kisasa wa Boko uliopo Boko nje kidogo ya Dar es
Salaam, ikiwa ni kilomita chache kutoka hoteli walipoweka kambi yao.
Hata hivyo, kocha mkuu wa Yanga,
Mholanzi Hans van Der Pluijm amesema kuwa ameukubali
ubora na uzuri wa uwanja huo na kutamani kuendelea kukifundisha kikosi chake
mpaka mwisho wa msimu huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment