Benchi
la ufundi la Mbeya City limesema kuwa limejipanga vilivyo kuhakikisha kiungo
mshambuliaji wa Simba, Ramadhani Singano ‘Messi’ hafurukuti katika mechi ya
kesho ya Ligi Kuu Bara itakayozikutanisha timu hizo kwenye Uwanja wa Sokoine
jijini Mbeya kwa kumwekea ulinzi wa kutosha.
Kocha
mkuu wa timu hiyo, Juma Mwambusi amesema kikosi chake kipo vizuri kwa mchezo
huo na mipango ya kuwadhibiti wasumbufu imekamilika.
“Tumejipanga
vizuri kwa mechi hiyo na ni matumaini yetu kuwa tutaibuka na pointi tatu ambazo
zitatusaidia kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi hii.
“Kuhusiana
na Messi ni mchezaji mzuri lakini tayari nimeshawapa majukumu vijana wangu,
endapo watafanikiwa kumdhibiti kama tulivyopanga tutaibuka na ushindi, kwani
yeye hivi sasa ndiye mpishi mkubwa wa mabao ya Simba,” alisema Mwambusi.
Aidha,
Mwambusi aliongeza kuwa hali ya mvua kunyesha mara kwa mara ilisababisha kukosa
muda mzuri wa kufanya mazoezi lakini hiyo haiwezi kuvuruga mipango yake ya
ushindi.







0 COMMENTS:
Post a Comment