Unakumbuka mshambuliaji Mrundi wa Simba, Amissi Tambwe alipiga
hat trick katika mechi dhidi ya Mgambo katika mzunguko wa kwanza?
Lakini kukabidhiwa mpira ikawa longolongo kutoka kwa TFF na
mwamuzi wa mchezo huo, leo hawakuwa na ujanja baada ya Mrundi huyo kupiga hat
trick yake ya pili katika Ligi Kuu Bara.
Wamemkabidhi mpira wake palepale uwanjani, tena kwa kutumia
bango la wadhamini, kitu ambacho si kawaida.
Eti mtu kukabidhiwa mpira tu lazima kuwe na bango wa wadhamini,
jiulize wadhamini hao ni wadhamini wa hat trick au vipi?
Au inawezekana kuwa siku ile hakukabidhiwa mpira kwa kuwa
hakukuwa na bango hilo uwanjani? Acha tubaki na maswali, ufafanuzi utapatikana
baadaye lakini leo Tambwe amekabishiwa mpira wake.
0 COMMENTS:
Post a Comment