KIKOSI cha Al Ahly ya Misri, kilianza
rasmi mazoezini jijini juzi Alhamisi ikiwa ni siku moja tu baada ya kuwasili nchini
kikitokea kwao Cairo, Misri.
Mazoezi ya mabingwa hao wa Afrika
yalikuwa yakifanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Kimataifa ya
Tanganyika (IST) iliyopo Upanga.
Lakini kama ilivyo ada, timu za Misri
zinapokuwa nchini zimekuwa na uoga wa hujuma, hivyo ilikuwa ni ‘full’ vituko.
Ulinzi ulikuwa mkali kupita kiasi
katika eneo linalozunguka shule hiyo, kwani Al Ahly iliwasili mazoezini hapo
ikiwa kwenye msafara unaongozwa na pikipiki ya askari wa barabarani inayopiga
king’ora.
Lakini uwanjani hapo, walinzi
walikuwa wakizunguka kila eneo la uwanja huo na maeneo mengine ya shule hiyo ili
kuhakikisha hakuna mtu yeyote anayepata upenyo wa kushudia mazoezi ya timu hiyo,
lakini Championi likawapiga bao, likashuhudia na kupata picha.
Waandishi na wapigapicha wa gazeti
hili walikumbana na wakati mgumu kutoka kwa walinzi hao katika siku zote mbili
walizofuatilia mazoezi ya Al Ahly.
Katika siku ya kwanza, Jumatano
iliyopita, baada ya kufika shuleni hapo kwa lengo la kutaka habari
pamoja na picha za mazoezi ya timu hiyo wandishi wa gaezeti hili
walizuiliwa na walinzi wa shule hiyo.
Walinzi hao waliokuwa wamesimamiwa na
jamaa mmoja ambaye alionekana kama ofisa wa ubalozi wa Misri hapa nchini
walisema kuwa wamekatazwa na viongozi wao kuwa mtu yoyote ambaye si hatakiwi
kuingia ndani ya uzio wa shule hiyo.
Baada ya kujadiliana kwa muda mrefu
kati ya walinzi hao na wandishi wa gazeti hili walikuja walinzi wengine na
kuwataka waondoke katika ene hilo.
“Tunaomba mwondoke katika eneo hili
kwani hamruhusiwi kuwa hapa nuda huu na tunawaomba msipoteza muda wenu hapa
hamuna yoyote atakayepata nafasi ya kushudia mazoezi haya hata kwa dawa,”
alisema mmoja wa walinzi hao huku wengine wakiwa wamenuna bila hata ya
kuonyesha meno yao.
Baada ya hali hiyo, waandishi wakajipanga na
kuzunguka nyuma ya uzio ambako kulikuwa na upenyo kidogo, wakapanga mawe na
kuanza kushuhudia mazoezi hayo.
Ili kupata picha safi zaidi, zoezi la
kupanga mawe haraka lilifanyika na picha ambazo ni exclusive zikapigwa “ta ta
ta”, kama unavyoziona kwenye ukurasa huu.
Jumatano:
Kikosi hicho cha Al Ahly kilifika
uwanjani hapo Saa 9.30 Alasiri kikiwa na msafara wa magari sita moja likiwa ni
basi, Kakore Trans lilokuwa limebeba wachezaji. Magari madogo yalikuwa
yamewachukua makocha na maofisa wa ubalozi wa Misri nchini.
Rasmi walianza mazoezi Saa 9.40 Alasiri
kwa wachezaji wa timu hiyo kuzunguka nusu uwanja mara 10 kisha wakanyosha
viungo na kuanza kuchezea mpira kwa kupigana pasi fupi fupi kwa muda wa dakika
15.
Baada ya hapo walibadili programu na
kuanza kurushiana mpira kama wanacheza Rugby kwa muda wa dakika 15. Wakanyoosha
viungo kisha wakanza kuruka koni.
Baada ya mazoezi hayo walinyosha tena
viungo na wakagawanya katika makundi mawili kisha wakanza kucheza mpira na
baada ya kumaliza mazoezi yao walikusanyika pamoja na kuomba dua, wakaondoka
zao.
Alhamisi:
Ulinzi ulikuwa wa hali ya juu zaidi ya
ule wa Jumatano, kwani walinzi walitawanyika semu mbalimbali za uwanja huo
kuhakikisha hakuna mtu yeyote anapata nafasi ya kushudia mazoezi hayo.
Hata ule upenyo ambao wandishi wa
gazeti hili waliutumia kupata picha pamoja kuona mazoezi ya timu hiyo Jumatano,
ulikuwa umezibwa kwa na kuwekwa mlinzi.
Lakini pamoja na hali hiyo wandishi
wa gaezti hili hawakukata tamaa, walendelea kupambana na kunawakati walijifanya
kuwa ni maofisa wa Shirikiho la Soka Tanzania (TFF), lakini mambo yalikuwa
magumu kwao.
Walinzi waliendelea kuweka ‘uso
mbuzi’ na kudai kuwa kama wangewaruhusu kuingia basi kazi zao ‘zingeota nyasi’
kwani kila kitu walichokuwa wakikifanya kilionekana kwenye kamera maalum za
ulinzi katika eneo hilo.
Juhudi za kusaka upenyo mwingine
zilianza, ukapatikana na kama kawa, picha zikapigwa tena na Championi kikawa
chombo pekee kilichopata picha zao mara mbili kwa siku mbili.
Katika mazoezi hayo Alhamisi, wachezaji
wa Al Ahly mara baada ya kufika uwanjani hapo, walianza kwa kupasha misuli
kisha kuzunguka uwanja mara sita na baada ya hapo walianza kuchezea mpira na
wakati huo viongozi wa benchi lao la ufundi wakijadiliana jambo.
Baada ya hapo waligawanywa katika makundi
mawili na kuanza kucheza soka kwa ushindani
wa hali ya juu na kocha wa timu hiyo alikuwa ikiandika kila kitu kilichokuwa
kikitokea uwanjani hapo.
Kunawakati walikuwa wakicheza soka la
pasi fupifupi lakini kunawakati walikuwa wakicheza pesi ndefu na wachezaji wa
timu moja katika mazoezi hayo walionekana kuwa wazuri kwa mpira hiyo.
Hata hivyo baada ya mazoezi hayo
yalioanza Saa 10:00 jioni na kumalizi Saa 11:30 walikusanyika na kuomba duwa kisha
wakaondoka zao.
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment