Yanga imesema haitahama njia kuu kuepuka
michepuko, hivyo imebaki njia kuu na kuweka rekodi mpya kwa kuifunga Al Ahly ya
Misri kwa bao 1-0.
Kabla Yanga haikuwa imewahi kuishinda Al
Ahly ambao sasa ni mabingwa wa Afrika.
Bao pekee la Nadir Haroub Canavaro
katika dakika ya 83, lilimaliza ndoto za Warabu hao wa Misri kunyanyasa kila
wanapokuwa Tanzania.
Mechi ilikuwa safi na kila timu ilicheza
kwa kujituma, lakini Yanga walipoteza nafasi nyingi za wazi za kufunga.
0 COMMENTS:
Post a Comment