KAVUMBAGU (KULIA) |
Mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga, Mrundi,
Didier Kavumbagu, ameikubali kasi ya mabao ya Mrundi mwenzake anayekipiga Simba,
Amissi Tambwe na kukiri kuwa msimu huu mshambuliaji huyo atatwaa kiatu cha
ufungaji bora wa ligi.
TAMBWE |
Tambwe ambaye pia ni raia wa Burundi amefikisha jumla ya mabao 17 akiwa
ndiye kinara huku akiwa tayari ameshaifikia idadi ya mfungaji bora wa msimu
uliopita, mchezaji kutoka Ivory Coast, Kipre Tchetche wa Azam FC.
Akizungumza na Championi Jumatano,
Kavumbagu alisema kwa sasa Tambwe yupo juu kutokana na spidi aliyonayo na kuna
kila dalili ya kutwaa kiatu hicho msimu huu.
Alisema kwamba yeye binafsi ameikubali
kazi ya Tambwe na kumsifu jinsi anavyoisaidia Simba kwenye suala la kuzifumania
nyavu.
Hata hivyo, Kavumbagu alikiri kukihitaji
kiatu hicho ambapo alisema kama
ikitokea Mungu akimsaidia na kufunga mabao mengi zaidi kwenye mechi zilizobaki,
itakuwa vizuri lakini kwa sasa anaangalia jinsi gani ataisaidia timu yake
kuibuka na ubingwa msimu huu kisha ufungaji bora utakuja baadaye.
“Hilo suala lipo wazi, Tambwe yupo
vizuri msimu huu, anakifanya kile kinachotakiwa tena kwa spidi kubwa, nafikiri
ufungaji bora safari hii unaweza ukatua kwake, ni halali kabisa kwa sababu
anachokifanya kinaonekana na vizuri mtu anapofanya kitu kizuri kumpa haki yake
kwa kumsifia,” alisema Kavumbagu.
0 COMMENTS:
Post a Comment