Kocha maarufu wa Hispania, Luis
Aragonés amefariki dunia leo alfajiri akiwa na umri wa miaka 75.
Aragone maarufu kama 'The Wise Man of
Hortaleza', mchezaji wa zamani na kocha wa timu ya taifa ya Hispania alikuwa na
sifa ya ubaguzi.
Kocha huyo aliwahi kumbagua Thierry
Henry na kusababisha apewe adhabu na Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa).
Aliifundisha Hispania tokea mwaka 2004
hadi 2008.
Mwaka 2008, Hispania ilibeba ubingwa
wa Ulaya ikiwa mikononi mwake na baada ya hapo, miaka ya Hispania kuchukua
makombe ikaanza.
Kwani mwaka 2010, Vicente del Bosque
akachukua Kombe la Dunia na 2012 akarudia kutwaa tena Kombe la Ulaya.
0 COMMENTS:
Post a Comment