Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic
amesema leo watashambulia zaidi kuliko mechi dhidi ya Rhino ya Tabora.
Simba inacheza na JKT Oljoro katika
mechi yake ya pili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.
Logarusic amesema kikosi chake
kitaongeza ufanisi wa kushambulia zaidi kutokana na maendeleo yao.
“Kama tumeshinda, tumepata pointi tatu
na tumeangalia cha kufanya zaidi.
“Mechi ya pili tunaweza kushambulia
zaidi kuliko ya kwanza, ingawa siwajui wapinzani lakini tunahitaji ushindi
zaidi,” alisema Logarusic.
Mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Bara
mzunguko wa pili, Simba ilishinda kwa bao 1-0 lakini ilijilinda zaidi.
0 COMMENTS:
Post a Comment