Kocha Mkuu wa AS Cannes, Jean Marc
Pilorget amesema zimebaki siku chache sana kama hajachoshwa na Shomari Kapombe.
Pilorget amesema alivutiwa sana na uwezo
wa Mtanzaia huyo, lakini kinachotokea sasa kinamkera.
“Nimekuwa nikiuliza kila mara kuhusiana
naye kama kweli atakuja huku lini, naambiwa ni kesho na imekuwa hivyo kila
siku.
“Mambo yanavyokwenda inaonekana mchezaji
pia ana matatizo, nitakuwa na subira kidogo tu.
“Sifurahishwi na mambo yanavyokwenda na
kama ikizidi hali hii, nitaangalia mipango mingine,” alisema.
Taarifa zinaeleza Kapombe amelipwa kila
anachodai na klabu hiyo lakini uamuzi wake umekuwa ni kubaki jijini Dar.
Wakati uongozi wa AS Cannes inayoshiriki
daraja la nne, umekuwa ukitaka arejee kazini mara moja .









0 COMMENTS:
Post a Comment