Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic
amekubali kuwa Mgambo JKT waliwapoteza katika mechi yao iliyopita.
Logarusic raia wa Croatia amesema Mgambo
JKT walistahili kushinda mechi hiyo ya juzi kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini
Tanga kwa kuwa walicheza vizuri.
“Walicheza vizuri sana, kwa kiwango
chetu hatukufanya vizuri katika mechi hiyo.
“Tumeliona hilo na tunaendelea na
maandalizi kuhakikisha tunafanya vizuri katika mechi zinazofuatia,” alisema.
Simba imepoteza mechi ya kwanza ya ligi
ikiwa chini ya Logarusic baada ya kufungwa na Mgambo bao 1-0.
Katika mzunguko wa kwanza, Mgambo
ilicharazwa na Simba kwa mabao 6-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar huku
Mrundi, Amissi Tambwe akiingia nyavuni mara nne.







0 COMMENTS:
Post a Comment