Kocha Mkuu wa Mbeya City, Juma Mwambusi
amesema wanawasubiri Simba kwa hamu.
Mwambusi amesema anawasubiri kwa hamu
katika mechi ya Ligi Kuu Bara itakayopigwa Jumamosi ijayo mjini Mbeya.
Simba itakuwa mgeni wa Mbeya City ambao
wamepoteza mechi moja tu kwenye Ligi Kuu Bara baada ya kufungwa bao 1-0 na
Yanga.
“Tunajua mechi itakuwa ngumu, Simba watakuwa
wamepania kutuangusha lakini kweli sisi tunasubiri kwa hamu.
“Tutaendelea kujiandaa na kikubwa
tunachotaka ni kushinda na mwisho ikiwezekana kutwaa ubingwa au kuiwakilisha
Tanzania katika michuano ya kimataifa,” alisema Mwambusi.
Mbeya City ambayo haijafungwa kwenye
Uwanja wa Sokoine, ilimaliza mzunguko wa kwanza bila ya kupoteza hata mchezo
mmoja.







0 COMMENTS:
Post a Comment