Kocha Mkuu wa Coastal Union, Ahmed
Morocco ametamba kikosi chake kitaishinda Simba leo.
Morocco aliyekuwa kocha wa Coastal Union
katika mzunguko wa kwanza amesema kama mwamuzi wa leo akiwa fair, Simba inalala
Uwanja wa Taifa Dar.
“Sisi tunachotaka mwamuzi achezeshe kwa
haki, halafu utaona, Simba hawatapona,” alisema.
“Tumejiandaa vizuri na tuna ari ya
kushinda. Tunajua Simba ni wazuri, lakini kwa sasa kikosi chetu ni bora zaidi,”
alisema.
Oljoro ilianza mzunguko wa pili kwa sare
ya bao 1-1 dhidi ya Coastal Union ikiwa ugenini mjini Tanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment