Mashabiki wa
Gor Mahia ya nchini Kenya wamemtumia salamu za rambirambi aliyekuwa kipa wa
timu hiyo, Ivo Mapunda, baada ya kufiwa na baba yake mzazi, Philip Mapunda, juzi.
Mauti ya
mzazi wa kipa huyo yalitokea Jumanne katika Hospitali ya Ikonda mkoani Njombe
na aliwatarajiwa kuzikwa jana Alhamisi katika Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.
Mashabiki wa
timu hiyo kupitia mitandao ya jamii wamesema wamepokea kwa masikitiko makubwa
taarifa za kipa huyo kuondokewa na mzazi wake mzee Mapunda ambaye aliugua kwa
muda mrefu.
“Tunampa pole
sana Mapunda kwa kuondokewa na baba yake tunafahamu yuko katika wakati mgumu
sana kwa sasa lakini ni kazi ya Mungu haina makosa bado tunamkumbuka sana huku
Kenya kwa kazi kubwa aliyoweza kuifanyia timu yetu,” alisomeka shabiki mmoja.
Ivo ambaye ni
kipa wa zamani wa Yanga, amekuwa pia katika wakati mgumu kwenye timu yake
ambapo amejikuta akiwekwa benchi katika mechi mbili zilizopita kutokana na
kudaiwa kucheza chini ya kiwango.
0 COMMENTS:
Post a Comment