Uongozi wa Mbeya City umesema unataka
kuhakikisha timu yao inashinda mechi zote za nyumbani zilizosalia katika msimu
huu wa Ligi Kuu Bara ambazo ni sawa na pointi 15 ili ifanikiwe kumaliza katika
nafasi mbili za juu katika ligi hiyo.
Kauli hiyo ya uongozi wa Mbeya City inamaanisha
kuwa kila timu itakayofika kwenye Uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya lazima iache
pointi zote uwanjani hapo. Timu hizo ni JKT Oljoro, Rhino Rangers, Prisons,
Azam FC na Mgambo.
Mwenyekiti wa Mbeya City, Mussa
Mapunda amesema wanaelekeza nguvu zao kwa mechi zilizobaki hasa za nyumbani kwa
kuhakikisha wanachukua pointi zote.
“Lengo letu kubwa ni kushinda mechi
zetu saba zilizobaki katika mzunguko huu wa pili na hatutakuwa tayari kupoteza
mchezo hata mmoja hasa katika mechi tano ambazo tutaweza kucheza katika uwanja
wa hapa nyumbani.
“Kuhusu suala la ubingwa bado lipo, hatujakata
tamaa kabisa tukifanya vizuri kwenye michezo yetu iliyobaki,” alisema Mapunda.
0 COMMENTS:
Post a Comment