February 28, 2014


Katika hali isiyokuwa ya kawaida mgambo waliowekwa getini kwenye Uwanjan wa Azam Complex uliopo Mbande.


Mgambo hao walimzuia Kanali Kanal Idd Kipingu kuingia uwanjani hapo kushudia mechi kati ya Twiga Stars na Zambia  kwa madai kwamba hawamtambui.


Hakukuwa na kiingilio, hivyo watu wakajitokeza kwa wingi hadi mgambo hao wakalazimika kuanza kuzuia watu.
Alipofika Kipingu, naye akazuiwa na juhudi za baadhi ya watu kwamba huyo ni kati ya watu wenye mchango mkubwa kwenye soka.
Bado mgambo walikomaa na ‘head’ na kuendelea kumzuia Kipingu anayesifika kwa mchango mkubwa wa kukuza vijana katika soka nchini.

 Hata hivyo kiongozi huyo na mwalimu mkuu wa zamani wa shule ya Sekondari ya Makongo ilibidi atumie kazi ya ziada kuwapigia viongozi wa TFF waliokuwa uwanjani hapo waje mlangoni kumsaidia kuingia.
Juhudi za Kanal Kipingu kuingia uwanjanbi humo zilizaa matunda dakika za lala salama maarufu kama fungulia mbwa ndipo kiongozi huyo alifanikiwa kuingia.

Akizungumzia tukio hilo Kipingu alisema hana cha kulaumu kama uongozi wa uwanja huo hivyo ndivyo walivyopangawala haina sababu ya kuwalaumu mgambo hao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic