Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq, amewaonya Yanga
kutobweteka na ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Komorozine ya Comoro.
Yanga
iliibutua Komorozine kwa mabao hayo saba katika mechi ya Ligi ya Mabingwa
Afrika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, juzi.
Akizungumza
mara tu baada ya mechi hiyo, Sadiq alisema Yanga hawapaswi kubweteka na ushindi
huo kwa kuwa wanakwenda kucheza ugenini.
“Sasa
wanakwenda ugenini, lazima wajiandae vizuri kwa ajili ya mechi ijayo. Hauwezi
kujua kwa kuwa mpira una mambo mengi.
“Hawa jamaa
wakati fulani walionyesha ushindani, hivyo Yanga wasione wamemaliza kazi, hadi
dakika 90 za kule Comoro zikiisha, basi ndiyo watakuwa wamemaliza kazi,”
alisema Sadiq aliyeshuhudia mechi hiyo kwa dakika 90.
Yanga
inajiandaa kwenda Moroni, Comoro kwenda kuwavaa Komorozine ambao walionyesha
kiwango cha chini hiyo juzi na wakivuka wanakutana na mabingwa wa Afrika, Al
Ahly.








0 COMMENTS:
Post a Comment