| SIKU ALIPOPOKELEWA NA MASHABIKI |
Kiungo mshambuliaji mwenye kasi, Emmanuel Okwi, amesema anaumia kuona anakaa nje
wakati timu yake ikipambana uwanjani.
Okwi, raia
wa Uganda, amesema ana hamu kubwa ya kuitumikia Yanga ambayo ina majukumu ya
kutetea ubingwa na kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Okwi amesema anatamani kuungana na wenzake na kupambana
kwa ajili ya Yanga.
“Nasikia
vibaya, naumia sana moyoni kwangu kuona nimekaa tu wakati nilitaka kucheza.
Naupenda mpira, achana tu na kazi lakini ndiyo mchezo ninaoupenda.
“Nataka
kucheza, nataka kuungana na wenzangu kuitumikia Yanga. Ndiyo maana nina hamu kuona
mambo haya yanaisha mapema,” alisema.
Okwi ambaye
usajili wake umesimamishwa na Shirikisho la Soka Tanzania (Fifa) hadi
litakapopata uhakika kutoka kwa lile la kimataifa (Fifa), amekuwa akishuhudia
mechi za Yanga akiwa jukwaani.
Mganda huyo
aliyewahi kuichezea Simba, amekuwa akiendelea na mazoezi na hivi karibuni
aliungana na wenzake kambini Bagamoyo, lakini kuhusu kucheza ataendelea
kusubiri kutoka TFF ambayo inasubiri kutoka Fifa.







0 COMMENTS:
Post a Comment