, Hivi karibuni kumekuwa na madai ya kutoridhishwa na mwenendo wa
timu, taatifa za hujuma ndani ya timu yetu ya mpira, uongozi na baadhi ya
wanachama.
Ni haki 'kwa nia njema tu ya wanachama kuhoji mwenendo wa timu yao pale
wanapoona-hairidhishi, Ni wajibu wa wanachama kuchanganua mawazo merna na mabaya. .
Ushindi au mwenendo mzuri WCl- timu unatokana na viwango vizuri, nidhamu na ushirikiano wa wahusika wote, Wachezaji, Walimu, Viongozi, Wanachama na wapenzi kwa ujumla.
Uongozi ulikutana na wachezaji, walimu, baadhi ya wanachama na
wapenzi na kuyazungumzia na kukubaliana kuhusu mapungufu yaliyojitokeza kwa
wahusika wote na kuchukua hatua ya kubadilisha technical bench yote na kutoa
adhabu na onyo kali kwa baadhi ya wachezaji walionyesha utovu wa nidhamu kwa kipindi
kilichopita.
Inasikitisha kuona kuwa baadhi ya wadau kwa kutumia vyombo vya
habari wanachochea na kutengeneza uhasama ambao kwa kweli haupo ama kwa faida zao
binafsi, au kwa kutumiwa
na watu wa nje kutuvuruga na kuondoa amani klabuni.
Habari zilizoandikwa na moja ya gazeti maarufu za kusema
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Kimataifa Ndugu Seif Ahmed kuwa si mwanachama
halali wa YANGA, eti
anahujumu timu na yupo kwa maslahi yake binafsi ni za uzushi na
hazina ukweli wowote.
Habari hizi zimelenga kuwakatisha tamaa na kuwavunja moyo
viongozi wetu ambao wapo mstari wa mbele katika kujenga YANGA. Watu hawa ni hatari sana
na hawaitakii merna
YANGA na wanafanya hujuma hizi kwa malengo ya kuwapandikiza
viongozi vibaraka wa kuidhoofisha timu yetu na kutimiza malengo yao binafsi. Uongozi
ungependa kutoa tahadhari kwa wanachama kuwa hizo ni mbinu chafu ambazo
zimelenga kutudhoofisha na
kutusambaratisha. Wachochezi hawa kwa nyakati tofauti wamekuwa
pia wakutuma ujumbe wa simu wenye vitisho na matusi kwa kiongozi huyu na baadhi ya
viongozi wenzake.
Tunatoa onyo kwa wale wote wanaotuma ujumbe wa simu wenye
uchochezi na matusi, kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao mara
watakapofanya hivyo tena.
Tunawaomba wadau wote wanamichezo na hasa wahariri wa michezo
kudhibiti matumizi mabaya ya watu au vyombo vya habari yanayochangia sana
kuzorotesha michezo nchini.
Uongozi unawaomba Wana Yanga kutulia na kutoa ushirikiano katika
kupambana na njama hizi ambazo zinawe a kutudhoofisha tusipokuwa waangalifu ili
tushindwe kufikia malengo yetu.
YANGA, DAIMA MBELE NYUMA MWIKO YANGA
YUSUF MANJI
Mwenyekiti
0 COMMENTS:
Post a Comment