Jose Mourinho amesema uwezo wa kamati ya
nidhamu ya Ligi Kuu England kumuona kiungo Yaya Toure hana kosa ni tatizo.
Kiungo huyo wa Man City alimkanyaga
mshambuliaji wa Norwich, Ricky van Wolfswinkel katika mechi ya Premiership.
Kutokana na hali hiyo sasa Yaya atakuwa
katika kikosi kitakachoivaa Chelsea katika mechi ya 16 ya Kombe la FA,
Jumamosi, City ikiwa nyumbani.
Ndiyo maana Mourinho amethubutu kusema
hivyo kwa kuwa iliaminika lazima Yaya angefungiwa.
Kamati hiyo pamoja na kumsalimisha
Yaya, imetoa adhabu kwa Craig Bellamy kwa kumshambulia kiungo wa Swansea, Jonathan
de Guzman.










0 COMMENTS:
Post a Comment