Zawadi za fedha
taslimu kwa washindi wa Kilimanjaro Marathon 2014 zimeongezwa hadi zaidi ya
shilingi milioni 40 na kuifanya mbio hii kuwa kati ya m io kubwa zaidi barani
Afrika.
Waandaaji wa
mbio hizo wametangaza kuwa washindi wa wa Kilimanjaro Marathon 2014 watajipatia
zaidi ya shilingi milioni 40 fedha taslimu kama zawadi.
John Addison,
Mkurugenzi Mkuu wa Wild Frontiers, waandaaji wa mbio hizo alisema katika
taarifa yake kwa vyombo vya habari jana kuwa mbali na washindi kujinyakulia
zaidi ya shilingi milioni 40 pia watapata fursa ya kujishindia zawadi nyingine
kabambe za kuvutia kutoka wadhamini wakuu Kilimanjaro Premium Lager kwa
kushirikiana na wadhamini shirikishi.
Alisema
washindi wa mbio ndefu za marathon ya kilomita 42 watajishindia jumla ya
shilingi milioni 20, na zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni 10 kwa
washindi wa nusu marathon huku washindi wa mbio za walemavu maarufu kama GAPCO
10km Marathon wakijishindia kiasi cha shilingi milioni 6. Washiriki wote
watakaomaliza mbio za kujifurahisha za Vodacom 5km Fun Run wataweza kujishindia
zawadi mbalimbali.
Addison alisema
kuwa mbio za mwaka huu zimesheheeni motisha mbalimbali za kuvutia ili kuongeza
idadi ya washiriki. Washindi wa kwanza kwenye mbio ndefu za kilomita 42
(Kilimanjaro Premium Lager Marathon) wanawake kwa wanaume watajinyakulia kiasi
cha shilingi milioni 4 kila mmoja, shilingi milioni mbili kwa washindi wa pili
na shilingi milioni 1 kwa washindi wa tatu. Washindi wa kwanza kwenye mbio
ndefu za nusu marathon (km 21) wanawake kwa wanaume watajinyakulia kiasi
cha shilingi milioni 2 kila mmoja, shilingi milioni 1 kwa washindi wa pili na
shilingi 500,000 kwa washindi wa tatu.
Addison
aliongeza kuwa medali na t-shirt zitatolewa kwa wanariadha 500 wa kwanza
kumaliza mbio za kilomita 42, wanariadha 2,200 wa kwanza kumaliza mbio za nusu
marathon na wanariadha 80 wa kwanza kumaliza mbio za walemavu. Washiriki
3,000 wa kwanza kumaliza mbio za kujifurahisha za Vodacom 5km Fun Run watapewa
t-shirts baada ya kumaliza mbio na watapata fursa ya kujishindia zawadi
mbalimbali za kuvutia kupitia droo.
Ili kuwapa
hamasa wanariadha wa Tanzania kufanya vizuri katika mbio hizi, Kilimanjaro
Premium Lager imetenga kiasi cha shilingi milioni 2 bama bonsai kwa wanariadha
Watanzania watakaovunja rekodi katika mbio hizi.
Mbio hizi
zinaratibiwa na kwa kushirikiana na Riadha Tanzania, Chama cha Riadha Mkoa wa
Kilimanjaro na Kilimanjaro Marathon Club huku zikidhaminiwa na Kilimanjaro
Premium Lager, Vodacom Tanzania, GAPCO, Simba Cement, KK Security, Keys Hotel,
TPC Sugar, TanzaniteOne, CMC Automobiles Ltd, Kibo Palace Hotel, RwandAir, FNB
Tanzania, UNFPA na Kilimanjaro Water.








0 COMMENTS:
Post a Comment