March 4, 2014


Msemaji  wa Ruvu Shooting, MAsau Bwire ametoa kali ya aina yake baada ya kuonekana akiwa amebeba simu nne kwa wakati mmoja.


Bwire ambaye kitaaluma ni mwanahabari, alionekana akiwa na simu nne mkononi alizokuwa akiranda nazo wakati wa uchaguzi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa) uliofanyika jana kwenye Ukumbi wa Water Front jijini Dar.

Bwire alionekana akikatiza kila sehemu na simu zake nne, hali iliyozua gumzo kati ya wapiga kura na wajumbe.

Mwenyewe hakuonekana kujali sana, wakati mwingine alikuwa akipokea simu moja baada ya nyingine, tena kwa mbwembwe kabisa.

Wakati fulani alionekana akiomba kura kwa baadhi ya wajumbe akiwa na simu zake hizo, hali iliyowashangaza wengi kwa kuwa ni vigumu mtu kumiliki simu nne kwa wakati mmoja.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic