March 4, 2014

BRUNO AKIWA NA MPENZI WAKE NJE YA SALON WANAYOIMILIKI

Mbabe wa enzi hizo, bondia Mwingereza, Frank Bruno ameamua kuwa mtengeneza nywele na amesema wazi anavutiwa sasa na kazi hiyo.

MWAKA 1996 ALIPOZICHAPA NA TYSON

Bruno ametupia picha yake kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter na kusisitiza anataka kufungua salon ya utengenezaji nywele, hivyo wadau wapendekeze jina.

Hali hiyo imeonyesha kuwashitua watu wengi ingawa Bruno ,52, mwenyewe ameonyesha kutojali hata kidogo kuhusiana na hilo.
Bruno amekuwa akishirikiana na mpenzi kuendeleza salon hiyo na sasa ameamua kufunguka kabisa kuwa anapenda kazi hiyo.

Alistaafu ngumi za uzito wa juu baada ya kudundwa na Mike Tyson mwaka 1996 hali iliyosababisha moja ya jicho lake kupata matatizo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic