Mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati
ya Yanga na Al Ahly kutoka Misri iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki imeingiza sh. 448,414,000.
Mapato hayo yametokana na watazamaji
50,202 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 7,000,
sh. 13,000, sh. 25,000 na sh. 35,000. Yanga ilishinda mechi hiyo kwa bao 1-0.
Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama
ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 68,402,135.59, gharama za
kuchapa tiketi ni sh. 10,343,219, waamuzi na kamishna sh. 14,665,930 na
matangazo sh. 15,679,000.
Uwanja sh. 50,898,557.31, gharama za
mchezo sh. 33,932,371.54, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF)/Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 33,932,371.54 wakati Yanga
ilipata mgawo wa sh. 220,560,415.01.
Nayo mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom
(VPL) kati ya Simba na Ruvu Shooting iliyochezwa jana (Machi 2 mwaka huu)
imeingiza sh. 20,610,000 ambapo kila klabu ilipata mgawo wa sh. 4,402,492
wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 3,143,898.31.
0 COMMENTS:
Post a Comment