March 31, 2014


Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Azam na Simba iliyochezwa jana (Machi 30 mwaka huu) Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam imeingiza sh. 26,455,000.


Lakini inaonekana ni mapato kiduchu sana kwa mechi kubwa inayowakutanisha Simba dhidi ya Azam FC.

Watazamaji 4,741 walikata tiketi kushuhudia pambano hilo ambapo Azam iliibuka na ushindi wa mabao 2-1. Viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.

Mgawanyo kwa mapato ulikuwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 4,035,508.47, gharama za kuchapa tiketi sh. 3,908,686 wakati kila klabu ilipata sh. 5,460,687.63.


Uwanja sh. 2,776,620.83, gharama za mechi sh. 1,665,972.50, Bodi ya Ligi sh. 1,665,972.50, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 832,986.25 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 647,878.19.

Lakini hii si ya kupita kimyakimya, kwa kuwa mapato yake ni kiduchu kupindukia na hii inatokana na mambo mawili.

Kwanza ni kufanya vibaya kwa Simba, mashabiki wamepoteza imani hivyo wanakwepa maumivu.
Pili ni mechi kuonekana na Azam TV. Hivyo mashabiki wanaweza kubaki nyumbani na kuangalia kwenye runinga.
Jiulize, timu zinafaidika sahihi kwa Sh milioni 100 kwa msimu. Je, Simba ingeshindwa kupata zaidi ya hizo kama mechi zake hazionyeshwi kwenye runinga.
Hapa kuna jambo la kujifunza kuanzia kwa viongozi wa klabu za ligi kuu hasa zile zenye mashabiki wengi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic