Mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Ligi
ya Mabingwa Ulaya kati ya Atletico Madrid dhidi ya Chelsea imemalizika kwa sare
ya bila mabao.
Mechi hiyo iliyomalizika punde kwenye
Uwanja wa Vincente Calderone jijini Madrid, Hispania ilijaa ufundi wa kila
aina.
Chelsea ndiyo ilipata pigo baada ya kipa
wake Peter Chech kuumia na baadaye nahodha wake, John Terry akaumia na kutolewa
pia.
Wenyeji ndiyo walitafuta nafasi nyingine
zaidi na kufanikiwa kupata kadhaa, lakini Chelsea walionekana kuzitumia vizuri
mbinu za Jose Mourinho katika ulinzi.
Mechi ya pili kwenye Dimba la Stamford
Bridge jijini London ndiyo itakayotoa jibu, timu gani itasonga fainali dhidi ya
Real Madrid au mabingwa watetezi, Bayern Munich ambao wanakutaka kesho kwenye
Uwanja wa Santiago Bernabeu jijini Madrid.
0 COMMENTS:
Post a Comment