April 4, 2014



 
HALL (KUSHOTO) WAKATI AKIWA AZAM FC
Mkurugenzi wa Ufundi wa Symbion Power, Stewart Hall, raia wa Uingereza ambaye alikuwa Kocha wa Azam FC, amefunguka kuwa Kocha Mkuu wa Mbeya City, Juma Mwambusi, anastahili kuwa Kocha Bora wa Ligi Kuu Bara kutokana na upinzani aliouonyesha akiwa na kikosi chake.


Hall amesema kuwa, uwezo waliofanikiwa kuonyesha mpaka walipofikia sasa ni mkubwa na Mwambusi ndiye anayestahili tuzo hiyo, pia timu yake ya Mbeya City nayo inastahili kuwa timu bora.
 
MWAMBUSI
Aidha, alisema kuwa ligi ya msimu huu imekuwa na changamoto na mabadiliko tofauti na msimu uliopita, hasa kwa timu ngeni zilizofanikiwa kucheza ligi kwa mara ya kwanza msimu huu kama ilivyokuwa kwa Mbeya City, zimeonyesha changamoto.

“Changamoto waliyoionyesha msimu huu ni kubwa sana, Kocha Mkuu wa Mbeya City, Juma Mwambusi anastahili kuwa kocha bora msimu huu kwa uwezo wake na kikosi chake mpaka hapo walipofika ingawa ligi haijamalizika.

“Hii imesaidia kwa kiasi kikubwa kuifanya ligi kuwa ya ushindani na mpaka sasa bado kiukweli bingwa hafahamiki kuwa atakuwa ni nani tofauti na misimu iliyopita ya ligi kutokana na ushindani mkubwa kuwepo,” alisema Hall.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic