Hatma ya mwamuzi aliyechezesha mechi kati ya Yanga na Mgambo JKT, Alex
Mahagi, inatarajiwa kujulikana wiki ijayo baada ya Kamati ya Maadili kujadili
matukio yaliyotokea kwenye michezo ya Ligi Kuu Bara.
Mwenyekiti wa Chama cha Marefa wa Soka Tanzania (Frat), Mwalimu
Nassoro amesema kamati ya Maadili itakutana kujadili masuala yote yanayohusu michezo
ya ligi kuu, pia kupitia malalamiko na kuyatolea maamuzi.
“Hata hilo suala la mwamuzi aliyechezesha mchezo wa Mgambo na Yanga
tutalijadili kwa kupitia mkanda wa video wa mechi hiyo ili kubaini yaliyotokea,”
alisema Nassoro.
Mgambo ilishinda mabao 2-1 katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja
wa Mkwakwani, Tanga, huku mchezaji Mohammed Neto wa Mgambo akitolewa uwanjani
kwa kadi nyekundu kwa kosa la kubishana na mwamuzi.
0 COMMENTS:
Post a Comment