BAADA ya muda mrefu wa kusubiri, hatimae timu ya wananchi Yanga wamefungua tena kabati lao la makombe. Mara ya mwisho Yanga wametwaa kombe ni lini? Miaka sasa imepita.
Kabla hata hawajamsajili Papy Tshishimbi. Sasa hivi ameondoka na yupo zake kwao. Safari hii wanalifungua kabati lao kwa furaha zaidi kwa sababu wametwaa kombe kwa kuwalaza watani zao na wapinzani wao wa karibu, Simba.
Hakuna furaha inayozidi kumfunga mtani Tanzania. Hata furaha ya kutwaa ubingwa haipendezi kama ya kumfunga mtani. Mara nyingine hata kukosa ubingwa haujali kama umemfunga mtani.
Sijui hii nadharia alituachia nani. Sijui huu utaratibu ulitoka wapi. Kama wewe unafahamu niandikie sababu.
Kama ilivokuwa kwa Simba, Yanga wanachukua hili taji bila ya uwepo wa wachezaji wao wengi wa kikosi cha kwanza. Bakari Nondo Mwamnyeto, Lamine Moro, Yassin Mustapha na Feisal Salum ni baadhi ya mastaa wa Yanga ambao hawakuwepo Zanzibar.
Kukosekana kwao kulitokana na sababu mbalimbali, wengi wakiwa katika majukumu ya timu ya taifa, wengine walipewa likizo kama Lamine Moro.
Hakukuwa na sababu ya kwenda na wachezaji wa kikosi cha kwanza kupambania milioni 15. Hii pesa hata hailipi mshahara wa wachezaji watano wa Simba au Yanga. Ingekua labda bingwa anachukua kitita kinachotosha walau kujiendesha kwa mwezi mmoja.
Simba isingekubali kuwaachia akina Chama na Bwalya waende likizo. Nadhani waandaji wa haya mashindano wanaweza kufikiria namna ya kuyaongezea thamani zaidi kwa kuongeza zawadi zaidi.
Tofauti na thamani, pia tumezidi kuona ukubwa wa tofauti iliyopo kati ya vilabu vya Zanzibar na Bara. Ni wazi kwamba vilabu kutoka bara vipo vizuri zaidi kushinda vilabu vya Zanzibar. Unaweza kutaja sababu nyingi za uwepo wa hii tofauti, lakini sababu kubwa ni moja, uwekezaji.
Unapozungumzia uwezekaji kichwani mwako linakuja neno moja tu. Lipi hilo? Pesa! Na hiyo ndiyo sababu ya tofauti kubwa iliyopo kati ya vilabu vya Zanzibar na bara. Wakati watu wa bara wakikazana kuweka pesa kununua wachezaji na kuendesha vilabu, bado watu wa visiwani wamebaki nyuma.
Sijui ni kwasababu gani hasa ukizingatia Zanzibar wapo matajiri wengi tu. Labda kwa kuwa bado hawaamini kuwa soka ni biashara inayolipa kuliko biashara nyingi sana duniani.
Mwisho kabisa naweza kuwazungumzia wachezaji wa Simba na Yanga waliopata nafasi ya kucheza katika kombe la mapinduzi. Kama nilivozungumza hapo awali, wachezaji wengi wa Simba na baadhi wa Yanga waliocheza Zanzibar ni wale wa kikosi cha ziada.
Hakuna mashindano mengi Tanzania, yanapotokea mashindano kama haya, ndiyo nafasi ya kuwakumbuka wachezaji wasiopata nafasi mara kwa mara. Kwa mchezaji anayejielewa hutumia nafasi kama hizi kumshawishi mwalimu kuwa anahitaji nafasi kwenye kikosi cha kwanza.
Nililiona hilo kwa wachezaji wengi wa Simba na Yanga. Walijitoa sana na kujituma sana kuwauliza waalimu kwa nini hawawapi nafasi mara kwa mara. Bado nawaza Cedric Kaze atamuambia nini Abdalah Shaibu Ninja atakapokuwa anamnyima nafasi hata ya benchi.
Kwa aliyoyafanya Zanzibar, hata viongozi waliolazimisha dili la Dickson Job watakuwa wanauma meno wakisema, “Kumbe Ninja angeweza tu kufanya kazi?” Ndivyo inavotakiwa kuwa kwa mchezaji mwenye kiu ya kucheza. Sitaki kumzungumzia Ibrahim Ajib, yeye anajua maisha aliyoyachagua.
Imeandikwa na Oscar Oscar ipo ndani ya Gazeti la Championi Jumamosi
Wala stori hii haina mantiki. Nilidhani Dickson Job amesajiliwa kupambana kupata namba kumbe kuzyia the so calked ninja? Ninja hawezi mpira wa kistaarabu, kwa matefa wenye weredi na hasa wa nje ya TZ ninja hamalizi dakika 10 anapewa red. Unadhani hilo jina lilitoka wapi?
ReplyDeleteDhana kuona bora kumfunga mtani kuliko ubingwa tulishamiachia UTOPOLO. Mnyama anawaza mashindano vyenye tija
ReplyDeleteMngejitoa mashindano
DeleteMgosi inaonesha kichwa chako hakiweki kumbukumbu,umesahau zile mechi za magumashi za Simba na Yanga zilizokuwa zinaandaliwa na watu fulani ndani ya Simba ili kuzima mihemko ya wanachama na wapenzi waliokuwa wanataka kuwatimua ambapo dili lilikuwa linachezeshwa na wachezaji kadhaa wa Yanga wanavuta mshiko baada ya hapo hakukuwa na kelele tena za kuutimua uongozi kisa tu Simba kamfunga Yanga.
DeleteYanga sio timu ya Mpira wa miguu no chama Fulani hv Cha kisiasa,Yani wao wakiifunga Simba Mpira ilikuwa was kihalali,Ila wait wakifungwa na Simba Mara utasikia bila makando kando hatufungwi,Mara sijui Kuna wazee walisema wamefungwa 5-0 eti sababu wao walivua kofia, Mara Simba wamehonga wachezaji wao,wakawaaminisha mpaka wageni eti Simba wanapulizia sumu vyumbani no Bora mjikite kwenye siasa Mpira hamjui na ndio Mana hata kimataifa Simba ndio timu pekee ya Tanzania ambayo inafanya vizuri toka zamani
DeleteWakishinda wao utasikia mwamuzi kachezesha vizuri kulikuwa hakuna makando kando hata Kama wamepewa penalti Kati Kati ya uwanja,Ila wakifungwa wao Mara wachezaji wetu wamehongwa, Sasa hiyo ni timu ya Mpira kweli hiyo hicho no chama Cha siasa kilichokuwa kwenye kivuli Cha football,wanafungwa Barcelona Ina Messi na wanapigwa 8 mtakuwa nyinyi na hao wacheza shoo wa koffi olomide
DeleteUna uhakika na hilo usemalo?
ReplyDeleteSimba na Yanga ni zaidi ya uzijuavyo,we baki kusubiri matokeo either ushangilie au unune
DeleteHuyo ni mwehu tu wanapolichukuwa wao ndio linakuwa na tija wakichukua wengine halina Tina wamesahau Mwaka Jana walipofungwa na mtibwa mume wao mudy alitangaza kujitoa kuwalea waliandamana kwenda kumbembeleza mpaka akaenda makonda kuwaombea Leo hii eti wanafikilia mashindano makubwa mungejitoa basi
ReplyDeleteMhh ebu nendeni kamsafisheni miguu baasha wenu mliyebeba kwenye machela
DeleteKombe la kunywea pombe ya kienyeji mnachachawaaa
ReplyDeleteHata kama ni la kuvutia shisha lakini ndo kombe tu!!!! Hakika nimependa utani wako usioambatana na matusi maana huo ndio utani unaotakiwa baina ya Simba na Yanga.Tunawasubiri mchukue kombe la kunywea Whisky mtakapopambana na Al Ahly,AS Vita Club na El Merreikh tuwapigie makofi ya pongezi
DeleteHapo nimekuelewa
ReplyDeleteUtopolo Wana hasira ukiligusia kombe lao pekee la msimu huu,ok Basi Haina shida tufanye hv kombe la mapinduzi ni kombe kuuuubwaaa!! Barani Afrika Yanga wanastahili pongezi kuuuubwaaa kwa kutwaa kombe la mapanuzi aah samahani mapinduzi,wameweka historia barani Afrika,Yanga ni hatareeee!nafikiri hapo watafurahi,maana tunajua wanailazimisha furaha lkn moyoni Wana majonzi
ReplyDelete