Beki wa Simba, Mrundi Gilbert Kaze, ambaye anatajwa kuwa kwenye orodha
ya wachezaji watakaotemwa na kikosi hicho msimu huu, amefunguka sababu ya
kushuka kwa kiwango chake na pengine kuwa moja ya sababu za kuondoka kwake
klabuni hapo.
Kaze ambaye alianza msimu vizuri mara baada ya kutua Simba mwanzoni
mwa msimu huu, amesema sababu kubwa ni kuwa majeruhi na yamemkosesha raha,
hivyo anajua kuwa kiwango chake kimeshuka.
Beki huyo aliyejiunga Simba akitokea Vital ‘O ya Burundi akiwa na Amissi
Tambwe ambaye amekuwa na msimu mzuri klabuni hapo, amesisitiza kuwa uwepo wake
nje ya uwanja umesababisha hata mashabiki kukosa imani naye.
“Kukaa benchi kutokana na majeraha niliyokuwa nayo kumeniathiri sana kiwango changu, kwani nina hofu kama nitapata timu nyingine kama Simba wakiamua kuniacha kwa kipindi hiki, kwani sijaonekana kwa kipindi kirefu nikiwa nacheza,” alisema Kaze.
Tokea kuanza kwa mzunguko wa pili, Kaze amekuwa akikaa benchi na
inaonekana Kocha Logarusic anawaamini zaidi mabeki Donaldo Musoti kutoka Kenya
na Joseph Owino raia wa Uganda.
0 COMMENTS:
Post a Comment