Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko
Logarusic amesema amekubaliana na Zacharia Hanspope na huenda akabaki Simba.
Logarusic amesema amekutana
na Hanspope ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba na wamezungumza
na kukubaliana.
“Nitabaki Simba kwa makubaliano
yetu hasa kama yatatekelezwa, nimezungumza na Hanspope, tumekubaliana.
“Lakini nalazimika kurudi
nyumbani kwanza, nitaondoka kesho asubuhi kwenda Croatia na baada ya hapo
nitasubiri makubaliano yetu,” alisema Logarusic.
Alipoulizwa walichokubaliana
na Hanspope ambaye imeelezwa anatarajia kugombea uenyekiti, alisema.
“Tumezungumza mambo mengi,
lakini vizuri mkawasiliana naye na kujua tulichokubaliana. Yeye ndiye anaweza
kuzungumza,” alisema, kocha wa zamani wa Gor Mahia ya Kenya.
Mkataba wake ulikuwa ni wa
miezi sita tu baada ya kuichukua Simba katika mzunguko wa pili.
Pamoja na kuiwezesha
kuitwanga Yanga katika mechi ya Nani Mtani Jembe, Logarusic alishindwa kutamba
kwenye Ligi Kuu Bara na kumaliza katika nafasi ya nne.
0 COMMENTS:
Post a Comment